Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wakati Bunge la Katiba leo linaanza kujadili sura mbili za
Rasimu ya Katiba ambazo zitalenga Muundo wa Muungano, Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) umewataka wajumbe wake kutokuondoka Dodoma hadi
kumaliza kujadili sura hizo.
Kwa mujibu wa ratiba ya Bunge iliyotangazwa Ijumaa
iliyopita na makamu mwenyekiti wa Bunge hilo, Samia Saluhu, leo wajumbe
wataanza kujadili sura ya Kwanza ya Rasimu ambayo inahusu Jina, mipaka,
alama, lugha na Tunu za Taifa.
Sura ya sita, inahusu muundo wa Muungano, vyombo
vya utendaji na mamlaka ya Serikali, nchi washirika na uhusiano wa nchi
washirika.
Katibu wa Bunge la Katiba, Yahya Hamis Hamad
alisema utaratibu wa kujadili rasimu kwa kuanza na sura hizo umetolewa
na Kamati ya Uongozi kwa kuzingatia kanuni ya 58 ya Bunge la Katiba.
Kanuni hiyo ya 58 (3) inasema kamati ya uongozi
itakuwa na majukumu ambayo ni “(a) kujadili na kuamua mambo yote
yanayohusu uendeshaji bora wa shughuli za BungeMaalumu na kamati zake.
“(b) kujadili na kupanga ratiba ya utekelezaji wa
shughuli za Bunge na (c) kujadili na kufanya uamuzi kuhusu masuala
yatakayohitaji usuluhishi na maridhiano”.
Tamko la Ukawa
Mjumbe wa Bunge hilo, John Mnyika akizungumza kwa
niaba ya Mwenyekiti wa Ukawa, Freeman Mbowe, alisema kuanzia leo Bunge
litaanza kujadili muundo wa Muungano ambao alisema ndiyo moyo ya Rasimu
ya Katiba hivyo wajumbe wote wa Ukawa watashiriki.
“Tumewaomba wajumbe kutokuondoka wakati wa
kujadili sura hizi mbili kwani ndiyo roho ya rasimu na tunaonya ikifikia
hatua CCM wakachakachua, tutachukua maamuzi (uamuzi) mazito na kwa
gharama zozote,” alisema Mnyika.
Mnyika alisema tayari wamepata taarifa kuwa
wajumbe kutoka CCM wataingia na mapendekezo yao na yatapigiwa kura kwa
kujua wao wapo wengi pamoja na uteuzi wa wajumbe 201 walioteuliwa na
Rais Jakaya Kikwete .
Hata hivyo alisema wakati wa kupitisha vifungu vya
rasimu hiyo ni wazi kuwa CCM haina theluthi mbili kwa Zanzibar na kama
wakipeleka mapendekezo ya kutaka kuvunja sheria na kanuni kwa masilahi
yao hawatakubali.
Mnyika alisema licha ya Mwenyekiti wa Kamati ya
Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kueleza upungufu wa mfumo wa
Serikali mbili na hivyo kupendekeza Serikali tatu ambayo ni maoni ya
wananchi, bado CCM inashinikiza na kutetea msimamo wao.
Mnyika alionyesha waraka aliodai wa siri wa CCM kuhusu jinsi ya
kupinga mapendekezo ya Sura ya Kwanza na ya sita katika rasimu hiyo.
Alionya kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya
kupitisha sura katika rasimu, ni lazima ipatikane theluthi mbili kwa
upande wa Tanzania Bara na kwa Zanzibar.
Tamko hilo la Ukawa limekuja siku chache baada ya
wajumbe wake kadhaa, akiwapo Mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema
kutangaza nia ya kuondoka Dodoma, akipinga mwenendo wa Bunge hilo hasa
upigaji wa kura za wazi na siri kwa wakati mmoja.
Lema alidai kwa mazingira yaliyojengwa bungeni amepoteza imani ya kupatikana kwa Katiba ya wananchi.

Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment