Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Katibu wa Bunge,Dk. Thomas Kashililah.
Kauli hiyo aliitoa jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa bunge hilo halina uwezo wa kuajiri madereva.
Dk. Kashililah alisema utaratibu wa kuwalipa madereva upo chini ya wajumbe wenyewe ambao wamekwenda Dodoma na watumishi hao.
“Sisi tunalipa posho ya Sh 230,000 kwa mjumbe kama perdiem na Sh 70,000 ndiyo posho ya kikao husika, lakini katika hesabu hiyo, pesa za dereva ni Sh. 30,000 na 30,000 ni kwa ajili ya mafuta,” alisema Kashililah.
Alisema jambo linalowafanya wasiingilie malalamiko hayo ni kutokana na ukweli kuwa hawakuweka sheria rasmi kwa mjumbe kuwa na dereva.
Kuhusu wajumbe ambao hawana madereva, alisema ni haki yake kupewa kiasi hicho na kubaki nacho kwa kuwa anatumia njia zake za kumrahisishia kufanya shughuli zake za bunge.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment