Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Jaji Fredrick Werema.
Akizungumza na NIPASHE, Werema alisema tangu kuanza kwa bunge hilo kumekuwa na matumizi ya lugha zisizofaa, zomea zomea na matendo mengine ambayo hayastahili kufanywa kwenye chombo hicho.
”Waache utoto, uvumilivu, wasome vizuri na kuzielewa kanuni, waelewe mahitaji ya Watanzania na wasome nyakati,” alisema.
Jaji Werema alisema kwa sasa unapozungumzia haki za binadamu haiwezi kufanyika sawa na miaka ya 70 au 90, na kwamba ni lazima kujua haki mpya za watu wachache ambao wanaishi kwa kula matunda, za watoto, wazee na vijana.
”Muundo wa Muungano ambalo linaonekana ni jambo kubwa lililobebwa kwenye Rasimu ya Katiba na wengi wamepeleka maoni, lazima tuwe makini, tuwe kwa kuacha hamaki, sikiliza hoja jenga hoja kama tulivyokuwa kwenye kamati,” alisema.
Jaji Werema alisema wakati wa mjadala wa kanuni ndani ya Kamati ya Kanuni na Kumshauri mwenyekiti, Tundu Lissu alisimama na kujenga hoja jambo ambalo linaonyesha kuwa iwapo wataacha ushabiki kwa kuwa Katiba si ya vyama bali ya Watanzania wote.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment