Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Baadhi ya Wajumbe wa Bunge la Katiba, wamewataka wenzao kuacha
kutoa tuhuma za kumlaumu, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
Jaji Joseph Warioba kutokana na Rasimu ya pili aliyoiwasilisha bungeni,
badala yake wajiandae kutetea misimamo yao.
Wakizungumza nje ya Viwanja vya Bunge Freeman
Mbowe, Silyvester Kasulumbai na Paul Kimiti, walisema alichowasilisha
Jaji Warioba bungeni,siyo maoni yake binafsi.
Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai,
alisema ni makosa makubwa kuanza kumlaumu Jaji Warioba, kwani
alichowasilisha ni maoni ya wananchi yaliyokusanywa yana tume nzima ya
Mabadiliko ya Katiba.
“Mzee Warioba pia ametumia taarifa za tume ambazo
iliundwa na Serikali na pia uamuzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), hivyo
kumtupia lawama yeye ni kumvunjia heshima yake”alisema
Mjumbe Kasulumbai ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Maswa Mashariki, alisema hakubaliani na wanaomlalamikia Jaji Warioba
kwani anaamini ametoa Rasimu ya umma.
Alisema kama angekuwa na uwezo , Rasimu ya Jaji Warioba ingepita kama ilivyo kwani inawakilisha maoni ya umma.
“Kama ni mimi ningeipitisha yote kama ilivyo kama
kurekebisha ni mambo madogo sana na nashangaa wanaomtuhumu na kumpinga
na wafuasi wenzake wa CCM,”alisema
Kwa upande wake Kimiti alisema anamheshimu jaji Warioba na alichofanya ni kuwasilisha bungeni maoni ya wananchi.
“Binafsi najua mzee Warioba ameeleza kwa uwazi
bila kuficha na haya ni maoni ya wananchi na utafiti wa uliofanywa
naTume hivyo muhimu ni kutafakari na kujiandaa kwa mjadala”alisema.
Tangu Jaji Joseph Warioba kuwasilisha rasimu
bungeni, kumeibuka mjadala mzito miongoni mwa wajumbe wa bunge la Katiba
na baadhi wamekuwa wakimpinga kwa madai sehemu kubwa ya maoni ni ya
Jaji Warioba.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment