Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Tisa, Samuel Sitta ameelezea
changamoto alizopata katika mchakato wa uchaguzi uliomweka madarakani
kuwa Mwenyekiti wa Bunge la Katiba baada ya kupata kura 487. Katika
uchaguzi huo, Sitta alimshinda mpinzani wake Hashim Rungwe kwa tofauti
ya kura 418. Awali Sitta alipata upinzani wa ndani ya chama kutoka kwa
aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge ambaye
alitajwa kutaka kuwania nafasi hiyo.
Upinzani huo uliibua mvutano mkali na kusababisha
makundi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo yalizimwa na uongozi
wa chama hicho kuwaita Sitta na Chenge na kuwataka wakubaliane nani kati
yao, asimame kugombea nafasi hiyo.
Sitta azushiwa ugonjwa
Baada ya Chenge kumpisha mwenzake Sitta awanie
nafasi hiyo na Samia Suluhu Hassan kuwa makamu wake, kulisambazwa
taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa Sitta ni mgonjwa mahtuti na
amepelekwa hospitali kwa matibabu.
Taarifa hizo zilianza kusambaa Machi 12 kuanzia
saa nne usiku, hali ambayo iliibua sintofahamu kwa baadhi ya wajumbe wa
Bunge hilo wanaomuunga mkono mgombea huyo.
Baada ya kurudisha fomu za kugombea nafasi hiyo,
Sitta alizungumzia uvumi huo na kusema, “Wabaya wangu ndio waliosambaza
hizo taarifa. Mimi ni mzima na nimetoka kurudisha fomu za kugombea
Uwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba.”
Anaongeza, “Mimi ni kiongozi ninayetenda haki kwa
kila mtu jambo ambalo linawaudhi watu wanaotaka kupendelewa kila jambo.
Sikushangazwa na taarifa hizo kwa sababu nilipoteuliwa na CCM kugombea
nafasi hii wapo waliopinga na kusema kuwa siwezi kugombea kwa sababu
mimi ni waziri.”
Sitta anasema kuwa licha ya kupitishwa na chama
chake kugombea nafasi hiyo, alishangazwa na kitendo cha aliyewahi kuwa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Terezya Huvisa
kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo.
“Huvisa ana nguvu fulani nyuma yake. Asingeweza
kuibuka tu na kukiuka uamuzi wa chama na kuchukua fomu za kugombea maana
kamati iliyonipitisha ilikuwa chini ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda,”
alisema.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment