Home » » KATIBA IONGEZE USAWA WAJINSIA KUWA TUNU YA TAIFA

KATIBA IONGEZE USAWA WAJINSIA KUWA TUNU YA TAIFA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mtandao wa  wanawake waharakati wa katiba wamelitaka bunge  maalumu la katiba kuongeza usawa wa jinsia kuwa tunu ya taifa.
 
Msemaji wa mtandao huo, Halima Sharif, alisema kwenye rasimu ya katiba inayojadiliwa bungeni zimetajwa tunu  saba, hivyo wanataka usawa wa kijinsia uongeze kwenye orodha hiyo.
 
Tunu hizo ni utu, uzalendo, uadilifu, uwajibikaji, uwazi, umoja, pamoja na Kiswahili.
“Tunalitaka bunge liongeze usawa wa kijinsia ili kuwiana na mkakati wa ushiriki wa  50 kwa 50 baina ya wanawake na wanaume, unaotajwa kwenye Protokali ya Maputo inayohimizia ushirikishwaji na fursa sawa kwa wote”, alisisitiza.
 
 Mwanamtandao mwingine, Asseny Muro, alisema mfumo wa sheria  haumpi mwanamke fursa ya kushiriki shughuli  za kimaendeleo.
 
“Mchakato wa katiba uzingatie usawa wa jinsia katika kumilikishwa rasilimali mbalimbali ikiwamo ardhi kwa sababu imekuwa ni moja ya sababu ya kumgandamiza mwanamke,”alisema Asseny na kuongeza  kuwa, kuendekeza mila na desturi potofu kuwa ni chanzo kingine cha kumkandamiza mwanamke.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa