Home » » Wafugaji wahofu Katiba kutowatambua

Wafugaji wahofu Katiba kutowatambua

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

KUNDI la wafugaji nchini wameeleza hofu ya maisha yao kutokana na rasimu ya pili ya Katiba kutokuwa na vipengele vinavyotambua uhalali wao wa kuishi na shughuli wanazofanya.
Akizungumza na Tanzania Daima juzi, Mwakilishi wa wafugaji ambaye ni mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Makeresia Jibubu, alisema baada ya kupitia rasimu hiyo wamebaini kuwepo na vipengele ambavyo havijaonyesha thamani ya wafugaji nchini.
Alisema katika rasimu hiyo wafugaji wametajwa katika kipingele cha malengo makuu na sera ya nchi na kusema ili suala la wafugaji liwe na umhimu linapaswa liwekwe kwenye kipengele cha wajibu na haki za binadamu, ili waweze kutambulika kisheria.

Chanzo;Tanzania Daima 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa