Wafanyakazi
walioajiriwa na shirika la Reli Tanzania (TRL) wakitoa mchanga kwenye
kichwa cha treni ya mizigo kilichopata ajali usiku wa kuamkia katika
stesheni ya Gulwe, Wilaya ya Mpwampwa. Katika ajali hiyo watu wawili
wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa na kulazwa katika hospital
ya Benjamin Mkapa Wilayani Mpwampwa.
Sehemu
ya mabehewa ya mafuta na ngano ambayo hayakusombwa na maji katika
ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika stesheni ya Gulwe, hiyo
imetokea saa 9.15 usiku. Treni hiyo ya Mizigo ilikuwa ikitokea Dar es
Salaam na kuelekea Mkoani Kigoma na ilikuwa na mabehewa yaliyobeba
ngano, sukari na mafuta.
Njia
ya Reli iliyoondolewa na maji katika stesheni ya Gulwe Wilaya ya
Mpwampwa kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha maeneno mbambali
nchini.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka akitoka kwenye maji
baada ya kuangalia kichwa cha treni kilichopata ajali na kusombwa na
maji katika stesheni ya Gulwe, Wilaya ya Mpwampwa, usiku wa kuamkia
juzi(Ijumaa), kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali
za nchi. Ajali hiyo imesababisha kifo cha watu wawili na wengine saba
kujeruhiwa na kulazwa katika hospital ya Benjamin Mkapa iliyoko wilayani
Mpwampwa.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk, Shaaban Mwinjaka akimfariji mmoja wa
Majeruhi wa Ajali ya treni ya mizigo iliyotokea katika Stesheni ya Gulwe
Bw. Michael Lupatu wakati alipomtembelea katika hospitali ya Benjamin
Mkapa iliyopo Wilayani Mpwampwa leo mchana. Ajali hiyo ya treni ya
mizigo imetokea usiku wa kuamkia juzi na kusababisha kifo cha watu
wawili na wengine saba kujeruhiwa.(Picha na kitengo cha Mawasiliano
Serikalini uchukuzi).
0 comments:
Post a Comment