Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba,Kangi Lugola.
Akizungumza na NIPASHE, alisema mjadala unaoendelea ndani ya Bunge hilo unaonekana ni mvutano wa kivyama na kwa wanaotaka kura ya wazi hawana lengo jema na wajumbe ambao wanatokana na vyama vya siasa.
”Mtu keshafukuzwa kwa kwenda kinyume na maagizo ya chama...tunakuja kujadili kanuni ya siri au wazi, halafu manalumbana,” alisema.
Lugola alisema kitendo cha kushindwa kuafikiana kwenye kanuni ya kura ya siri au wazi ni ishara ya kushindwa mapema na watu hawataki kuacha itikadi zao.
”Tutunga Katiba za vyama, kwanini tumeshindwa kuafikiana kwenye kura ya wazi au siri, hata kama tumeweka kiporo tukirudi tutarudi pale pale na watu hawataki kuacha itikadi zao, mapepo yale yale ya kiitikadi yatarudi...hatutahafikiana mana kilichotufanya tushindwe kufikia mwafaka ni kuweka itikadi katika utungaji wa kanuni,”
alisema.
Lugola ambaye ni Mbunge wa jimbo la Mwibara (CCM), alisema wingi wa kupitisha kanuni umetokana na vitisho, hivyo Katiba itakayopatikana itakuwa ya vitisho.
”Wingi unaotokana na vitisho, unaona watu wananyanyuka na kuunga mkono kanuni mbovu, ndiyo huo huo utakaopitisha Katiba mbovu na matokeo yake itakuwa Katiba imetokana na vitisho, kwa mara ya kwanza Tanzania tutapata Katiba inayotokana na vitisho,” alisema.
Alisema kwenye makundi mbalimbali wanapokutana wanaweka misimamo na baadhi kupeana vitisho na kwamba ni wachache ambao hawaogopi vitisho kwani asilimai 95 ya mwanadamu anaogopa vitisho.
”Mbunge wa Viti Maalum kwenye kata ana wapiga kura watano ya 30, ni lazima anavyotishwa na chama chake akunje mkia,” alisema.
Alisema ndani ya Bunge hilo na nje kila akitafuta fursa ya kuweka bayana msimamo wake, unawekewa alama, jambo ambalo linatia woga.
Alisema tangu awali alitabiri mwenyekiti wa muda, Pandu Ameir Kificho, hatalifikisha Bunge hilo salama kwa kuwa vifungu vya maamuzi vimewekwa viporo kutokana na Mwenyekiti kuyumba.
”Mwenyekiti wa muda aliyumba na hajatufikisha salama, sidhani kwa mwenyekiti huyo huyo ambaye anahudhuria vikao vya chama na anaona msimamo wa chama chake,” alisema.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment