Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mjumbe wa Bunge la Katiba, Kangi Lugola ameapa kuwa atakufa na
tai shingoni kwa kuitetea hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, Jaji Joseph Warioba kwa kuwa ndiyo iliyobeba mawazo ya watu
wengi.
Kutokana na hilo, Mbunge huyo wa Jimbo la Mwibara
anaonekana kutofautiana waziwazi na Mwenyekiti wa chama chake cha CCM,
Rais Jakaya Kikwete ambaye aliipinga baadhi ya vipengele vya rasimu
hiyo.
Akizungumza baada ya kupangwa kwenye kamati,
Lugola alisema kuwa haoni tatizo katika hotuba ya Warioba na kwamba
atakuwa wa mwisho kuisaliti.
Alisema kuwa mawazo ya Tume ya Jaji Warioba ndiyo
mawazo ya Watanzania walio wengi ambao walipendekeza kuhusu Katiba
wanayoitaka.
“Sasa mkisema napingana na Mwenyekiti wangu,
nadhani siyo dhambi kufanya hivyo kama tunapingana kwa misingi ya hoja,
lakini msimamo wangu mimi ni Serikali tatu ambayo ndiyo hotuba ya
Warioba aliyesimama pale kwa niaba ya watu wote,” alisema Lugola.
Alisema kuwa Katiba anayoitaka ni ile iliyotoka
kwa wananchi na wala siyo Katiba inayotoka kwa viongozi na kuongeza hata
Mwenyekiti wa CCM (Rais Kikwete) atakuwa analijua hilo.
Mbunge huyo machachari alisema kuwa mbali na
kupangwa katika kamati ambayo imejaa vigogo wakubwa wa CCM hatajali na
kuapa atapambana hadi mwisho.
Mwenyekiti wa Bunge Samuel Sitta alitangaza orodha ya majina kwa kila kamati jana na Lugola amepangwa kamati namba 6.
Hata hivyo, huenda akapata upinzani mkubwa
kutokana kamati hiyo kuwa na vigogo wa CCM, Sophia Simba, Stephen
Wasira, John Magufuli.
Vigogo wengine wa CCM walioko kwenye kamati hiyo
ni pamoja na Margareth Sitta, Dk. Fenela Mukangara. Pia yumo
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema jambo
linalodhihirisha atapata wakati mgumu.
Tangu kuanza kwa Bunge la Katiba, Lugola amekuwa
na msimamo wa kuunga mkono Serikali tatu yeye pamoja na Mbunge wa
Nkasi, Ali Keissy.
Chanzo;Tanzania Daima
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment