Home » » Mambo ya Muungano hayakuongezwa kinyemela-JK

Mambo ya Muungano hayakuongezwa kinyemela-JK

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Dk. Emmanuel Makaidi (kushoto) akibishana na mjumbe mwenzake, David Mathayo walipokuwa wakitoka kwenye Ukumbi wa Bunge hilo, mjini Dodoma jana.

Rais Jakaya Kikwete amesema mambo ya Muungano yaliongezeka kutoka 11 mpaka 22 kwa makubaliano kati ya pande zote mbili za Muungano.
Katika hotuba yake bungeni, Rais alisema siyo kweli kwamba mambo hayo yaliongezwa kwa hila au kutokana na udhaifu wa viongozi wa Zanzibar katika kutetea masilahi ya nchi hiyo.
Alisema kabla ya jambo lolote kuongezwa kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano, palifanyika makubaliano na mapendekezo ambayo yalipelekwa bungeni na kujadiliwa.
Rais Kikwete alitoa historia ya namna mambo hayo yalivyoongezwa kwenye Muungano na kutaja kuvunjika kwa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa na moja ya sababu ya mambo ya Muungano kuongezwa mara kwa mara.
Alisema mambo tisa kati ya 11 yaliyoongezeka yalitokana na kuvunjika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais Kikwete alitaja sababu nyingine ya ongezeko la mambo ya Muungano kuwa ni mabadiliko ya mfumo wa siasa, mwaka 1992 kutoka chama kimoja kwenda vyama vingi. “Ni mambo mawili tu yaliyotokana na uamuzi na makubaliano ya nchi washirika wa Muungano,” alieleza.
Hata hivyo, alibainisha kuwapo kwa baadhi ya mambo ambayo mbali na kutajwa kwenye Muungano, yanashughulikiwa na Zanzibar. Aliyataja kuwa ni Bandari, Utafiti, Utabiri wa hali ya hewa, Leseni za biashara na Takwimu na kwamba imethibitika inayamudu.
Rais Kikwete alibainisha kuwa walishakubaliana na Rais Mstaafu Aman Abeid Karume na kwamba hata sasa wakati wa uongozi wa Dk. Mohammed Ali Shein, makubaliano hayo bado yapo hai. Kilichokuwa kikisubiriwa kuyatangaza, ni wakati mwafaka ambao alisema ni sasa.
Alishauri maboresho ya rasimu bungeni yazingatie kuwa masuala ya uchumi na kuwa makini na athari za uamuzi wa kuchukua muundo mpya wa Muungano.
Chanzo;Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa