Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mvutano unaoendelea ndani ya Bunge Maalum la Katiba unachangiwa
kwa kiasi kikubwa na makundi yasiyo rasmi ya wanasiasa ambayo kwa bahati
mbaya yanatambuliwa na Uongozi wa Bunge hilo.
Madai hayo yametolewa na Mwenyekiti wa Baraza la
Vyama vya Siasa Tanzania, Peter Kuga Mziray, katika mkutano na
wanahabari uliofanyika mjini Dodoma leo.
“Uwepo wa makundi haya na kutambuliwa kwake na
bunge kunachochea mgawanyiko na kujenga uhasama baina ya wajumbe wa
Bunge Maalum la Katiba,” alisema Mziray.
Hali hiyo imevuruga “dhana ya kufanya kazi pamoja”
na kupelekea mashauriano yakwame, amesema Mziray, ambaye pia ni mjumbe
wa Bunge la Katiba anayewakilisha Vyama vya Siasa.
Aliongeza: “[Majadiliano] yanakwama kwa sababu
kamati ya uongozi kama imejaa wana CCM watupu, kila watakachokuja nacho
pale kitakataliwa.”
Mwakilishi wa Vyama vya Wakulima Dk. Maselle Maziku anaamini tatizo haswa ni wanasiasa, na si vinginevyo.
“Vyama vya kisiasa vimekuwa vinafikia muafaka
katika mambo mbalimbali na kutoa taswira kwamba kuna muelekeo mzuri,
lakini baadae wanasiasa haohao wanabadilika na kuyabadili maridhiano
hayo na kuanzisha mijadala mipya inayoturudisha nyuma.”
Maria Sarungi-Tsehai, anayewakilisha Mjumbe toka
Taasisi Zisizokuwa Za Kiserikali anafikiri wajumbe wengi hawawathamini
Wananchi waliowatuma Bungeni hapo, la sivyo wasingeendelea kuibua
mijadala ambayo imeshasuluhishwa.
“Tumepoteza hela za walipa kodi wiki 3 tunajadili
kanuni tu, sasa kwa nini turudi wakati [tumeshapata] kamati, tunataka
kuanza kazi, kwa nini tena suala la kanuni liibuliwe?” alihoji.
“Hapa watu hawana huruma na pesa za walipakodi.”
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment