Home » » Mambo ya maji hayatakuwa katika Katiba

Mambo ya maji hayatakuwa katika Katiba

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Waziri wa Maji,Profesa Jumanne Maghembe amesema, masuala ya maji na vyanzo vyake yatazungumziwa katika sheria na si katika Katiba inayotakiwa kuandikwa kwa kifupi.
Profesa Maghembe aliyasema hayo jana mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Wiki ya Maji inayofanyika mkoani Dodoma, kuanzia Jumatatu ijayo.
Profesa Maghembe alisema, Katiba ni sheria mama inayotakiwa kubeba masuala ya msingi na kwa msingi huo mambo mengine yataelekezwa katika sheria.
“Ukianza kuandika kila kitu katika Katiba utajikuta unakuwa na kitabu kikubwa ambacho hata kubebeka hakibebeki…masuala mengine yanatakiwa kuwekwa katika sheria ambayo ndiyo inaweka utekelezaji wake,”alisema Profesa Maghembe.
Pia alisema katika kuhakikisha kuwa vyanzo vya maji vinalindwa kikamilifu, wizara yake iko mbioni kukamilisha mapendekezo ya marekebisho ya sheria itakayoongeza kiwango cha adhabu kwa waharibifu .
Chanzo;Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa