Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Balozi Mustafa Nyang’anyi, amesema kushuka kwa uzalendo, uchu wa
madaraka na chuki miongoni mwa Watanzania, ndiyo mambo yanayowasukuma
baadhi ya watu kupiga kampeni ya kutaka muundo wa Serikali tatu.
Amesema hata hivyo, kampeni hizo ni sawa na
kukashfu fikra za waasisi wa Taifa la Tanzania, Hayati Baba wa Taifa
Mwalimu Nyerere na Hayati Mzee Abeid Aman Karume. Balozi Nyang’anyi,
aliyasema hayo katikati ya wiki hii, alipokuwa akizungumza na gazeti
hili kijijini kwake Kisese, wilayani Kondoa, Dodoma.
Alisema Muungano ni sawa na ndoa ambayo daima
haiwezi kukosa changamoto na kwamba kwa msingi huo, watu badala ya
kufikiria kuliongezea Taifa mzigo wa kugharimia Serikali tatu, ni vyema
wakabaki na Serikali mbili.
Balozi Nyang’anyi alisema waasisi wa Muungano
waliamua kwa makusudi kuwa na muundo wa Serikali mbili na kwamba
walitanguliza mbele uzalendo kwa maslahi ya Tanzania.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment