
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime - SACP
Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia mtu mmoja aliyekamatwa
huko katika kijiji cha Nga’mbi kitongoji cha Mgaye Wilayani Mpwapwa
akiwa a silaha tano (5) aina ya Gobore pamoja na zana za kutengenezea
silaha za aina hiyo.
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna msaidizi
mwanandamizi wa Polisi DAVID MISIME amesema anayeshikiliwa ni BAHATI S/O
MWANDACHE mwenye miaka 65, Mkaguru, Mkazi wa NGA’MBI.
Kamanda
MISIME amesema mtu huyu ni mtengenezaji wa wa silaha za aina hiyo
ambazo uchunguzi wa awali umebaini kuwa hutumiwa pia na wahalifu
wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu ikiwemo uwindaji haramu.
Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani wakati wowote kujibu tuhuma zinazomkabili.
Kamanda
MISIME anawashukuru wananchi kwa jinsi wanavyoshirikiana na Jeshi la
Polisi kuweza kuwafichua waharifu na kuzuia uhalifu kwa kutoa taarifa
mbalimbali za uhalifu na wahalifu.
0 comments:
Post a Comment