Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAZIRI Mkuu,
Mizengo Pinda kesho atakuwa mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi Tuzo
ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013-14, itakayowakutanisha wanawake wanne
itakayofanyika kesho katika Ukumbi wa The African Dream mjini Dodoma.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Global Publishers, ambayo ndiyo iliyoratibu zoezi hilo,
Eric Shigongo, alisema jana kwamba shughuli hiyo itakuwa ni hitimisho la
kazi kubwa ya kupokea na kuchuja kura zilizotumwa na wasomaji kumtafuta
mwanamke bora ambaye ni nembo kwa taifa.
“Zoezi
hili lilifanyika kwa muda wa miezi tisa, kuanzia Juni mwaka jana hadi
Machi mwaka huu. Awali kabisa watu walitakiwa kutuma majina ya wanawake
wanaowaona ni bora ili wapigiwe kura, watu waliitikia vizuri sana, kwani
jumla ya majina 150 yalitumwa katika kipindi cha miezi miwili.
“Baada
ya hapo majina hayo yakaandikwa katika magazeti na watu wakatakiwa
kupiga kura ili kuwatoa wanawake ambao wanadhani hawakustahili tuzo
hizo,” alisema Shigongo, ambaye kampuni yake inatoa magazeti ya Uwazi,
Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Amani, Risasi na Championi.
Alisema
katika awamu ya kwanza ya miezi hiyo miwili, majina ya wanawake 20
yaling’ara na hivyo kuingia katika awamu nyingine ya kupigiwa kura,
ambapo baada ya muda kama huo pia, wanawake kumi walipata alama nyingi
na hivyo kuingia katika awamu ya tatu na ya mwisho.
Alisema
kwenye hatua hiyo ya mwisho, wanawake watano walipita ambao ni Ananilea
Nkya, Anna Tibaijuka, Anna Kilango Malecela, Asha Rose Migiro na mama
Maria Kham. Katika zoezi hilo, wanawake hao wenye mvuto katika jamii
walichuana na mmoja wao, Nkya, kuondolewa baada ya kura zake kutotosha
kwa ajili ya fainali,” alisema Shigongo.
Kwa
upande wake, mratibu wa Tuzo hizo, Luqman Maloto, alisema tukio hilo la
kihistoria ambalo pia litashuhudiwa na wabunge wa Bunge la Katiba walio
mjini Dodoma, litaambatana na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali,
akiwemo Linah,” alisema Maloto.
0 comments:
Post a Comment