Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mjumbe wa Bunge la Katiba, Profesa Benadetha Kilian amekerwa na
tabia ya wanasiasa ya kuteka mjadala wa katiba akisema kitendo hicho
kitazaa Katiba mbovu.
Profesa Kilian alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki
alipokuwa akichangia hotuba ya Seneta Amos Wako alipolihutubia Bunge
hilo kuhusu historia ya namna nchi ya Kenya ilivyoweza kutengeneza
katiba yao.
Kiliani alionyesha mashaka makubwa akisema kuwa
hadi sasa dalili zinaonyesha kuwa mchakato wa katiba unabebwa kwa
seheumu kubwa na wanasiasa jambo linaloonyesha kufunikwa kwa mawazo ya
wengine.
Msomi huyo alimtaka Wako kutoa maelezo ya kina kwa
wajumbe ni namna gani nchi ya Kenya ilivyofanikiwa kupunguza nguvu ya
wanasiasa na kuruhusu mawazo ya makundi mengine.
“Kuna tabia ya wanasiasa na vyama vya siasa kuteka
nyara mawazo na michakato ya watu wengine, ningependa kujua kwa uzoefu
wako katika nchi yetu mlitumia njia zipi katika kupunguza makali ya watu
hao,”alisema Kiliani.
Alitahadharisha wajumbe wenzake kuwa makini na
masuala ya wanasiasa katika mchakato mzima wa utungwaji wa katiba kwa
kuwa inaweza kusababisha kuficha kabisa mawazo ya wananchi.
Akitoa ufafanuzi wa hoja hiyo, Seneta Wako alisema
kuwa katika maeneo mengi suala la wanasiasa katika utungwaji wa katiba
haliepukiki.
Wako alisema kitu cha msingi kinachowezaa
kuangalia ni jinsi gani mawazo ya wananchi yameingizwa na kupewa nafasi
yake kuliko kulundika mawazo na mitazamo ya wanasiasa.
Aliwataka wajumbe wa bunge hilo kuangalia jinsi ya
kuingiza mawazo ya wanasiasa lakini yakiwa nyuma ya mawazo ya wananchi
ambao ndio wenye katiba.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment