Home » » Ukawa wasaka viongozi wa kudumu

Ukawa wasaka viongozi wa kudumu

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Wajumbe wa Bunge la Katiba, ambao ni Wanachama wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wanatarajia kufanya uchaguzi wa kudumu Jumapili hii kupata viongozi wapya.
Katibu wa muda wa Ukawa ambao siku za karibuni, wamejipatia umaarufu mkubwa katika Vikao vya Bunge la Katiba, Julius Mtatiro, aliliambia gazeti hili kuwa uchaguzi huo, utafanyika kwa kujumuisha makundi yote.
Mtatiro alisema hadi sasa Ukawa ina wanachama 286 kutoka vyama vyote vya siasa na katika kundi la wajumbe 201 walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete.
“Kwa muda mfupi tangu tumeanzisha Uwaka kwa ajili ya kutetea maoni ya wananchi yaliyopo kwenye Rasimu ya Katiba tumekuwa na mafanikio makubwa katika kusimamia kanuni za Bunge”alisema Mtatiro.
Alisema moja ya mafanikio ni kuhakikisha Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba,anapata muda wa kutosha kuwasilisha rasimu tofauti na ilivyokuwa imepangwa.
Alisema katika uchaguzi huo, wanatarajia kupata viongozi kutoka katika makundi yote ambayo yamewakilishwa katika Bunge la Katiba.
Viongozi wa muda ambao wataongoza Ukawa ni Mwenyekiti James Mbatia, Katibu Julius Mtatiro makamu Mwenyekiti ni profesa Ibrahimu Lipumba na viongozi wengine ni Freeman Mbowe na Tundu Lissu ambao wamekuwa wakiitisha vikao mara kadhaa bungeni
Chanzo;Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa