Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wajumbe wa Bunge la Katiba wameelezwa kuwa ndani Bunge hilo
hakuna Waziri Mkuu, Makamu wa Rais wala mawaziri, wote wana hadhi sawa.
Hayo yalisemwa bungeni na Mjumbe wa Kamati ya Kanuni ya Bunge hilo, Ussi Jecha Sima, alipokuwa akijibu maswali ya wajumbe.
“Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na
Kanuni tulizozitunga humu ndani, hamna mawaziri, wote hapa ni wajumbe
wote tuna hadhi na status (nafasi) sawa,” alisema.
Awali akichangia semina hiyo ya kanuni, Luis
Majaliwa alisema, juzi wakati Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta,
alipokuwa akiahirisha Bunge alimwomba Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutoa
hoja ambayo iliungwa mkono na mawaziri walioko katika Bunge hilo.
“Kwa sababu katika Bunge la Jamhuri wanaopaswa
kuunga mkono hoja ni mawaziri, je,katika Bunge hili ambapo tupo mawaziri
wa Bunge la Muungano, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kundi la 201
ni utaratibu gani unaopaswa kutumika?” alihoji.
Chanzo;Mwananch
Chanzo;Mwananch
0 comments:
Post a Comment