(Picha na Maelezo-Dodoma)
(Na Magreth Kinabo-
MAELEZO,Dodoma)
Umoja wa Watumiaji wa Ardhi umewataka wajumbe wa Bunge Maalum
la Katiba kuanza kuifanya kuichambua Rasimu ya Katiba Mpya kama walivyotumwa na
wananchi ili kufikia malengo
yaliyokusudiwa na kuacha kufanya kampeni
za kufatuta madaraka kuliko kusimamia maslahi ya wananchi.
Kauli hiyo imetolewa leo na
Mwenyekiti wa umoja huo , Dk. Maselle
Maziku katika mkutano na
waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma .
Amesema umoja huo utafanya
kazi ya ya kuhakikisha unatetea haki za wakulima ,wafugaji na wavuvi katika
mchakato wa kujadili Rasimu ya Katiba Mpya.
“ Tunawataka wanasiasa watambue kwamba katikaBunge hili, hatukuja kufanya mabishano yasiyokuwa na
mwisho na badala yake tunataka tuanze kuifanya ile kazi ambayo wananchi
wametutuma ya kupitia na kuichambua
Rasimu ya Katiba,” alisema Dk. Maselle .
Aliongeza kuwa umoja
huo , umegundua kwamba makundi ya wanasiasa yanavuruga mchakato wa Bunge
hilo kwa kuendekeza misimamo yao ya
kiitikadi na kusahau azma iliyowaleta ya
kuhakikisha Watanzania wanapata Katiba
Mpya isiyokuwa na upendeleo wa chama chochote
cha siasa.Hivyo umeshoshwa na
hali ya Bunge hilo kuonekana kuwa ni sehemu ya makundi ya wanasiasa.
0 comments:
Post a Comment