Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mjumbe wa Bunge la Katiba, John Shibuda juzi aliwaacha hoi
wajumbe wenzake wanaotetea haki za wafugaji, wakulima na wavuvi, baada
ya kueleza kuwa kwa miaka 27 sasa, Serikali ya Tanzania na chama tawala,
vinaongozwa na Maazimio ya Kimataifa ya Magharibi badala ya kufuata
katiba.
Shibuda, akichangia mada juu ya marekebisho ya
Rasimu ya Katiba kuhusu kuongezwa suala la ardhi katika rasimu, alisema
kwa muda mrefu wajumbe wa Bunge hilo wamekuwa wakilalamikia dhuruma
ambazo zinafanyika katika maeneo yao.
“Nimekaa hapa kuwasikiliza wajumbe nimebaini mengi
ambayo mnayasema si mambo ya kuwekwa kwenye Rasimu ya Katiba, bali ni
malalamiko na manung’uniko juu ya dhuruma ambazo zinatokana na nchi hii
kuacha kufuata Sheria na Katiba na kuongozwa na Maazimio ya Kimataifa,”
alisema.
Alisema kama wafugaji, wakulima na wavuvi,
wanataka kuingiza hoja zao hasa suala la ardhi kwenye rasimu, ni muhimu
kwanza kujenga hoja nini malengo ya Katiba juu ya ardhi na waungane kwa
pamoja kusimamia vitu vichache.
Awali Mkurugenzi wa Shirika la Pingos Forums,
Edward Porokwa alisema wakati akitoa mada yake kuwa ni muhimu wajumbe wa
Bunge hilo kupitia kamati zao kujiandaa na hoja zenye nguvu katika
kushinikiza suala la ardhi kuingizwa kwenye rasimu
Chama;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment