Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wakati viongozi wa dini wakipaza sauti kutaka maoni ya wananchi
kuheshimiwa, Kanisa Katoliki Jimbo la Dodoma, leo litaendesha sala
maalumu ya kuliombea Bunge Maalumu la Katiba.
Ibada hiyo ambayo itafanyika saa 7 mchana katika
kanisa lililopo ndani ya maeneo ya Bunge, itaendeshwa na Askofu wa Jimbo
la Dodoma, Mhashamu Askofu Gervas Nyaisonga.
Kuendeshwa kwa ibada hiyo maalumu, kulitangazwa
bungeni mjini Dodoma jana na Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la
Katiba, Samiah Suluhu Hassan.
“Atakuja kusali katika kanisa la hapa bungeni saa 7
mchana kwa lengo la kuliombea Bunge Maalumu…Wakristo wote tunaombwa
kujumuika katika sala hii,” alisema.
Ibada hiyo inaendeshwa zikiwa zimepita siku chache
tu baada ya Maaskofu 32 wa kanisa hilo kutoa waraka maalumu wa Pasaka
kwa wajumbe wa Bunge hilo wakiwataka kuheshimu maoni ya wananchi.
Maaskofu hao walisema ili kupata Katiba bora,
wajumbe wanapaswa kuheshimu kazi ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na
kuitumia kama ilivyokusudiwa na sheria.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment