Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
“Pamoja na lugha ya kejeli inayotumiwa na Serikali kuniita mnafiki,
busara ya kawaida ilitakiwa kutumika kufanya maandalizi ya kuwarudisha
wajumbe nyumbani na kuandaa makabidhiano
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji
Joseph Warioba amesema waliokuwa wajumbe wa tume hiyo hawajawahi kudai
malipo ya pensheni ya Sh200 milioni kama inavyodaiwa.
“Wajumbe wa Tume hawajatoa madai ya kulipwa
shilingi milioni mia mbili. Hakuna mjumbe yeyote aliyetoa dai kama hilo
na Serikali inajua,” alisema
Jaji Warioba katika taarifa yake kwa vyombo vya
habari jana, aliyoitoa kupitia Nyalali, Warioba and Mahalu Law Advocates
ali ongeza:
“Nimeona taarifa iliyotolewa na Serikali kuhusu
Tume ya Mabadiliko, nimeshangazwa na maudhui na lugha iliyotumika,”
alisema Warioba akirejea taarifa iliyotolewa na Ikulu juzi ikieleza
jinsi tume hiyo ilivyohitimisha kazi zake.
Wiki hii Jaji Warioba alikaririwa akilalamika
jinsi yeye na makamishna wake walivyoondolewa ofisini na kunyang’anywa
magari kwa haraka bila kusubiri siku waliyopanga kufanya makabidhiano,
lakini Ikulu ilimjibu kwamba shughuli za Tume hiyo zilikoma siku ambayo
Tume ilivunjwa.
Katika taarifa yake ya jana, Jaji Warioba alisema
aliwasilisha Rasimu ya Katiba Machi 18 mwaka huu na Tume ilivunjwa Machi
19 wakati wajumbe wakiwa bado mjini Dodoma.
“Pamoja na lugha ya kejeli inayotumiwa na Serikali
kuniita mnafiki, busara ya kawaida ilitakiwa kutumika kufanya
maandalizi ya kuwarudisha wajumbe nyumbani na kuandaa makabidhiano,”
alisema.
Alisisitiza kuwa Serikali ilikuwa na wajibu wa
kuwarejesha makwao wajumbe wa tume hiyo, hata kama muda wa kisheria wa
kufanya kazi ulikuwa umepita.
“Niliwasilisha Rasimu Machi 18, 2014. Tume
imevunjwa Machi 19, 2014 wakati wajumbe wako Dodoma. Pamoja na lugha ya
kejeli iliyotumiwa na Serikali na kuniita mnafiki, busara ya kawaida
ingeonyesha umuhimu wa Serikali kujipa muda wa kufanya maandalizi ya
kuwarudisha wajumbe nyumbani,” alisema Jaji Warioba na kuongeza:
“Hata kama sheria ilitaja muda wa kuvunja Tume
bado ilikuwa ni wajibu Serikali kufanya mipango ya safari ya wajumbe
baada ya kumaliza kazi. Sheria haikuizuia Serikali kufanya hilo. Huo ni
wajibu wa Serikali na utaratibu wa kawaida unaotumiwa na Serikali kwa
tume zote inazoziunda. Inaonekana Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliwekewa
utaratibu tofauti. Kulikoni?”.
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment