Home » » KAMATI ZA BUNGE ZA BUNGE MAALUM ZAANZA KAZI VIZURI

KAMATI ZA BUNGE ZA BUNGE MAALUM ZAANZA KAZI VIZURI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

zendi 

Na        Magreth Kinabo – Dodoma
 Kamati 12 za Bunge Maalum  zimeaanza kazi vizuri ya  kuchambua Rasimu ya Katiba, huku baadhi ya wenyeviti wakisema kuwa muda wa siku mbili wa kujadili sura ya kwanza na ya sita  hautoshi.
 Hayo yamebainika  katika mahojiano  ya Mwenyekiti wa Kamati namba 11 ya Bunge hilo, Anne Kilango Malecela, yayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa St. Gasper  mjini Dodoma.
“ Tatizo lililojitokeza ni kwamba muda wa siku mbili hautoshelezi , leo tumejadili  sura ya kwanza sehemu ya kwanza kesho tutajadili sehemu ya  pili ya sura ya kwanza hivyo tunaweza tusiiguse sura ya sita.
“ Wenzetu walikakataa Kanuni zisirekebishwe. Lakini  wenzetu wapinzani wameliona hilo wameanza kusema muda hautoshi,” alisema  Anna .
 Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo atamweleza Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samwel Sitaa (leo jioni ) kuwa  muda hautoshi.
 Mwenyekiti huyo  tatizo lingine lililojitokeza katika  kamati yake ni baadhi ya wajumbe kutokuwa na uelewa wa tofauti ya dola na nchi, hali iliyomfanya kutumia kanuni namba 56(7) kumwomba Mwenyekiti wa Bunge hilo  ikiwezekana  kumleta  mtaalamu wa sheria ili kuweza kutoa elimu hiyo  leo (jioni) juu ya masula hayo.
 Akizungumzia kuhusu mjadala alisema wajumbe wote walijitayarisha vizuri na walishindana kwa hoja hivyo hakuna aliyetoa maneneo makali.
Akizungumza kwa njia ya simu na waandishi wa habari nje ya ukumbi huo, kwa sababu alikuwa katika  Mwenyekiti wa  Kamati namba moja ,Ummy Ali Mwalimu alisema  wajumbe walichangia kwa   utulivu.
 Ummy  alisema kilichojitokeza katika kamati yake ni kuwa muda hautoshi  kama ilivyodaiwa na baadhiya wajumbe kutoka upinzani, chama tawala na kutoka 201.
Naye  Mwenyekiti wa Kamati  ya  namba tano ya Bunge hilo ,Hamad Rashid  alisema kamati yake mjadala unaendelea vizuri na ulikuwa wa kistaarabu.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa