Home » » MKOA WA DODOMA ASHIRIKI SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA BODI YA HUDUMA ZA MAKTABA NCHINI MKOANI DODOMA‏

MKOA WA DODOMA ASHIRIKI SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA BODI YA HUDUMA ZA MAKTABA NCHINI MKOANI DODOMA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 
 Mkuu wa Mkoa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi (mwenye kilemba kichwani) akifanya ukaguzi wa vitabu na nyaraka za taarifa mbalimbali kwa ajili ya wasomaji , pembeni yake ni Mkutubi msaidizi wa maktabaa hiyo Ndg. Judith Lugongo, ukaguzi huo ulifanyika mapema Leo hii wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya bodi ya huduma za maktaba mkoa wa Dodoma.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi (mwenye kilemba kichwani) akikagua jengo la maktaba mkoa wa Dodoma kujionea mfumo wa vifaa vinavyotumika kutolea elimu na taarifa mbalimbali kwa njia ya video na sauti,  zoezi hili la ukaguzi lilifanyika mapema leo kwenye viwanja vya maktaba ya Dodoma wakati wa maadhimisho  ya miaka 50 ya bodi ya huduma za maktaba
 Watumishi wa maktaba ya mkoa Dodoma wakiwa tayari kupokea wananchi wenye mahitaji mbalimbali ya huduma za maktaba kwa ajili ya kuwapa maelekezo ya namna ya kupata taarifa na huduma nyingine mbalimbali mapema leo wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya bodi ya huduma za maktaba, maadhimisho mkoa Dodoma yalifanyika viwanja vya maktaba ya Dodoma.
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr Rehema Nchimbi (mwenye kilemba kichwani) akikagua nyaraka na vitabu mbalimbali wakati akitembelea mabanda ya maonesho  ya vitabu wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya bodi ya huduma za maktaba Nchini, maadhimisho mkoa Dodoma yalifanyika viwanja vya maktaba ya mkoa.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi (mwenye kilemba kichwani) akipata ufafanuzi kutoka kwa mtaalamu wa kutafsiri taarifa za vitabu na nyaraka mbalimbali katika lugha za watu wenye mahitaji maalumu/wenye ulemavu wa kuona (nukta nundu) Mwl. Charles Mtimatuku mapema wakati anatembelea mabanda ya maonesho wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 50 ya bodi ya huduma za maktaba nchini  mkoani Dodoma. Huduma za maktaba nchini zimepiga hatua kiasi cha kuzalisha taarifa na nyaraka mbalimbali kwa watu wenye mahitaji maalumu.
Baadhi ya walimu na wanafunzi shule za Dodoma waliojitokeza kwenye viwanja vya maktaba ya mkoa Dodoma kushiriki maadhimisho ya miaka 50 ya bodi ya huduma za maktaba nchini wakifuatilia salamu za mkuu wa mkoa Dodoma mapem leo.

NA JOHN BANDA

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa