Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Vyama vya upinzani vimeanza kutafuta utaratibu wa kuhakikisha
theluthi mbili kwa Zanzibar haipatikani katika kupitisha vifungu vya
Rasimu ya Katiba vinavyokwenda kinyume na matakwa ya wananchi.
Hayo yalisemwa na Mjumbe wa Bunge la Katiba, Hija Hassan Hija alipokuwa akizungumza na gazeti hili bungeni mjini Dodoma.
“Hawawezi kupata theluthi mbili, sisi Wawakilishi
na Wabunge kutoka vyama vya CUF na Chadema kutoka Zanzibar tunafikiria
kupiga kura za wazi ili tuweze kudhibiti kura zetu,” alisema Haji,
ambaye ni Mwakilishi kutoka Jimbo la Kiwani.
Alisema kama wajumbe wote 67 wanaotoka Zanzibar
katika kundi la wajumbe 201 hawatakubali kuburuzwa, CCM bado hawawezi
kupata theluthi mbili katika kupitisha uamuzi wa vifungu ambavyo
wananchi hawavitaki.
Haji alisema hata kama Rais Jakaya Kikwete atasema
kuwa wawape mambo wanayodai kupewa ikiwamo mapato yanayotokana na gesi
na haki ya Zanzibar kujiunga na nchi wanazozitaka, hawatakubali kwa
sababu wamekuwa wakiahidiwa kwa miaka 50 bila utekelezaji.
“Miaka 50 yote tumekuwa tukitaka kupewa haki zetu
za kujiunga na nchi mbalimbali, lakini hatukupewa iwe leo watupe sisi?
Hatutakubali Muungano huu, labda waseme wanatupatia muundo wote wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment