Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mjumbe wa Bunge la Katiba, Ismail Jussa Ladhu anaendelea kulia na Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta kuwa anawaburuza.
Jussa alitoa kauli hiyo katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma alipozungumza na gazeti hili.
Alilalamikia uongozi kuwa umepanga kuliburuza Bunge hilo.
Anacholalamika mjumbe huyo ni namna ambavyo
wamekuwa wakitafuta nafasi za kuchangia lakini Mwenyekiti anatoa nafasi
kwa wachache na kuwaacha wajumbe ambao wanatoka upande wa upinzani.
Jussa alisema wakati wanapitisha Kanuni, wajumbe
wengi ambao ni wabunge na wajumbe kutoka Baraza la Wawakilishi
hawakupewa nafasi ya kuchangia kutokana na kuwa walikuwa ni wajumbe wa
CUF.
“Nikikupa orodha utaona mwenyewe kwamba katika
upande wa CUF, alipewa nafasi Rukia Kassim pekee licha ya kuwa tuliomba
zaidi ya 10,” alisema Jussa.
Hata hivyo, Sitta alikanusha tuhuma hizo na
kusema shida inayowakumba baadhi ya wajumbe ni kutiliana mashaka
pasipokuwa na ushahidi.
“Hapa watu wanatiliana mashaka bila ya kujua
kinachoendelea mbele, hatuwezi kupanga orodha kama anavyosema mjumbe
katika masuala ya Kanuni, wakitaka wasubiri kwenye Rasimu, hivi sasa
kila kitu kinazuka palepale,” alisema Sitta.
“Wajumbe wa CCM walipewa zaidi ya nafasi tano, huu ni uonevu,” alisema Jussa.
Alimtuhumu Sitta kuwa anapendelea na kugawa nafasi
hiyo kwa wajumbe wa CCM pekee jambo linalotoa tafsiri kuwa, wamelenga
kupata Katiba ya upande mmoja.
Alilalamikia kitendo cha Mwenyekiti wa Bunge
kutogawa orodha ya wachangiaji wakati kanuni zinasema hivyo, jambo
analosema linamfanya Mwenyekiti kupoteza sifa.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment