Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, James
Lembeli ameapa hatakuwa tayari kubadili msimamo wake kuhusu Muundo wa
Muungano badala yake atasimamia kauli yake kwamba ukamilifu wa Tanzania
ni kuwa na Serikali ya Tanganyika.
Lembeli alisema kuwa, kauli aliyoitoa kuhusu kura
ya siri itabaki hivyo hadi mwisho wa kuchangia Rasimu ya Katiba kwa kuwa
ndicho anachokiamini.
Mwishoni mwa wiki wajumbe walipitisha kanuni ya 37
na 38 ambazo zilileta utata mkubwa ndani ya Bunge la Katiba hadi
ikapendekezwa kuwapo kura mbili kwa wakati mmoja.
Hata hivyo, wakati hayo yakitokea, Lembeli hakuwapo ndani ya Bunge hivyo hakuweza kupiga kura kuonyesha msimamo wake.
“Ni ukweli kwamba siku ya upigaji wa kura
sikuwapo, lakini kama ningekuwapo bado ningeendelea kusimamia msimamo
wangu huo hadi mwisho kwamba nataka kura ya siri,” alisema Lembeli.
Alisema suala la kura ya siri ndio msimamo wake
ambao amekuwa nao siku zote akiamini kuwa ndio utakaotoa haki kwa
wananchi wa Kahama kufikisha mawazo yao.
Kuhusu tetesi kuwa wana CCM wanaopinga uwapo wa
kura ya wazi wanaweza kushughulikiwa, mjumbe huyo alisema: “Hakuna wa
kumshughulikia mwenzake, isipokuwa ni Mwenyezi Mungu peke yake mwenye
uwezo huo.”
Kwa mujibu wa Lembeli, anacholilia katika kura ya
siri ni kutaka Tanganyika isimame na kupewa hadhi yake hata kama si kwa
masuala yote.
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment