Home » » NEWS: NAIBU WAZIRI WA FEDHA MWIGULU NCHEMBA AFUTA POSHO ZOTE ZA WABUNGE WALIOSUSIA KIKAO JUZI

NEWS: NAIBU WAZIRI WA FEDHA MWIGULU NCHEMBA AFUTA POSHO ZOTE ZA WABUNGE WALIOSUSIA KIKAO JUZI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 
Naibu Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Lameck Nchemba
Ikiwa ni Siku ya pili tangu Wajumbe wa Bunge la Katiba Kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo,Cuf na
NCCR Mageuzi wanaounda kitu kinachoitwa UKAWA wasusie Shughuli za Bunge la Katiba kwa Madai wamechoka Kutukana na Kuburuzwa kwenye Bunge hilo.
Hii leo Naibu waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba ambaye kwa Sasa anakaimu Kuwa Waziri wa Fedha tangu Tarehe.10./04/2014 hadi 18/04/2014 kutokana na Waziri wa Fedha kusafiri Nchini Marekani Kikazi,amefuta Malipo ya wabunge waliosusia Mchakato wa Katiba.
Habari za Uhakika Kutoka Chanzo chetu ndani ya hazina kinasema,Mwigulu Nchemba ameagiza Mabenki yote kurudisha Cheque za Malipo ya Posho na seating allowance zilizopelekwa na Bunge jana tar.16/04/2014 ili ziwekwe kwenye akaunti binafsi za Wabunge ikiwa ni Malipo ya Mpaka tar.20/04/2014.Pia ilikujiridhisha na taarifa hizo,Mwandishi wetu alizungumza na Wajumbe namna Mtiririko wa Malipo unavyofanyika ndani ya Bunge hilo,Mjumbe(Jina tunalihifadhi) alisema fedha zote zinapitia Benki na wakati wanajiandikisha siku za Kwanza walitakiwa Kuandika namba zao za Benki na Malipo yote hupitia huko,hivyo kama ni fedha zinazuiliwa Benki.

Baadhi ya wabunge wa CUF na Chadema wanaojiita UKAWA toka jana walijua wameshasaini fedha hizo hivyo zitaingia kwenye account zao Binafsi. Mambo yamekuwa tofauti baada ya Naibu Waziri wa Fedha(Sera) Mh:Mwigulu  kuagiza leo form zisainiwe upya leo na zitasainiwa pia tar 22 mpaka 25,Kwa madai ya asiyefanya kazi na asile. 
Mbali na hilo,Mh:Mwigulu amenukuliwa na clouds fm akisisitiza Rais kuwafuta wajumbe wakiojitoa na badala yake awateue watu waliotayari kutunga katiba hata bure kuliko hawa wanaokutana vikao lukuki kupanga njama za kususia mchakato. Aidha Mwigulu alisema fedha inayotumika ingeweza kulipwa Wazabuni wanaozidai halmshauri, wangeweza kulipa madeni ya walimu, au kuwapa mikopo watoto wa masikini waliofaulu ila hawajaenda vyuo kwa kukosa mikopo, au zingenunua madawa hosipitalini, au zingepeleka umeme, maji, vitabu au barabara lakini wamelipwa wajumbe badala ya kufanya kazi hiyo wanapanga njama ya kuhujumu mchakato usiendelee kwa kutafuta visingizio lukuki.
Bunge la Katiba linategemewa kuendelea Tar.22 Mwezi huu mara baada ya sikukuu za Pasaka Kupita na litaahirishwa tena Tar 25 mwezi huu kupisha Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Chanzo: Dj Sek Blog

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa