Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MKUU wa Wilaya ya Kongwa, Alfred Msovela, amesema kuna uwezekano wa
taifa kuingia katika machafuko kutokana na kuwepo kwa matabaka ya
wenye nacho na wasiokuwa nacho.
Alisema kutokana na wachache kuwa na maisha mazuri huku wengi kuwa na
maisha mabaya ndiko kumesababisha baadhi ya watu kuona bora kuishi
mijini na wengine vijiji.
Msovella alitoa kauli hiyo jana wakati wa uzinduzi wa mradi wa TASAF
awamu ya tatu uliodhamiria kupambana na kaya maskini zaidi nchini
zikiwemo zile za Wilaya ya Kongwa.
Alisema kuna kauli mbalimbali zinazomtambulisha mtu anayeishi
kijijini kama mkulima na kudai kuwa kilimo ni uti wa mgongo na kauli
mbalimbali bila kujali kuwa mkulima huyo anatumia nyenzo gani katika
kuendeleza shughuli zake.
“Wapo viongozi ambao wanadhani kuwa na wakulima wengi ndiyo kuwa na
wakulima wenye maisha bora na wazalishaji wa chakula cha kutosha,
kimsingi wakulima wanaweza kuwa wengi lakini wakaendelea kuwa maskini
kutokana na kutoweza kulima kisasa, wanalima kujikimu,” alisema
Msovella.
Akizungumzia kuhusu misaada ambayo inatolewa na TASAFIII kwa familia
maskini alisema atapambana na watumishi ambao wataonekana kufanya
udanganyifu kwa kushindwa kuwafikia walengwa.
Kwa upande wa uongozi wa TASAF, wamesema kuwa katika mradi huo
wanakusudia kuwaondolea umaskini watu milioni 7.5 nchi nzima sawa na
kaya milioni 1.2.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment