Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
KAYA milioni 1.2 zinatarajiwa kufikiwa na mpango wa serikali wa
kusaidia kaya masikini awamu ya tatu (TASAF III) ili kuzinusuru katika
Wilaya ya Chamwino, Dodoma.
Akizungumza kwenye warsha ya kutoa uelewa kwa madiwani na watendaji
wa halmashauri hiyo, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TASAF, Zuhura
Mdungi, alisema mradi huo unatekelezwa kwa kipindi cha miaka 10 katika
awamu mbili za miaka mitano mitano.
“Utekelezaji wa mpango huo unahitaji uwekezaji mkubwa kwenye mifumo
na kujenga uwezo katika ngazi zote. Utatekelezwa kwenye maeneo machache
na kuongeza kadiri ya uwezo unavyojengeka,” alisema Zuhura.
Akielezea kuhusu madhumuni ya mpango huo, alisema ni kuwezesha kaya
masikini sana kuongeza matumizi muhimu kwa njia endelevu, kuziwezesha
kwa matumuzi ya lazima ya binadamu na kuwekeza kwenye rasilimali watu,
hususan kusomesha watoto.
Madhumuni mengine ni kuimarisha shughuli za kuongeza kipato na
matumizi ya huduma za jamii huku akibainisha kwamba Rais Jakaya Kikwete
alizundua mpango huo Februari 2013 mkoani Dodoma.
Kwa mujibu wa mwakilishi huyo, mpango wa kunusuru kaya masikini
umeganyika katika maeneo mbalimbali ambayo ni kutoa ruzuku kwa kaya
masikini sana, hususan zenye wajawazito na watoto ili zipate elimu na
afya, lakini pia kutoa ajira kwa kaya zenye watu wenye uwezo wa kufanya
kazi wakati wa majanga mbalimbali.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment