Home » » WAJUMBE WA KAMATI MBALI MBALI ZA BUNGE WAENDELEA NA VIKAO MJINI DODOMA

WAJUMBE WA KAMATI MBALI MBALI ZA BUNGE WAENDELEA NA VIKAO MJINI DODOMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mjumbe wa Kamati namba kumi na mbili ya Bunge Maalum la Katiba Goodluck Ole - Medeye akichangia jana mjini Dodoma wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta alipoitembelea Kamati hiyo kujionea kazi inayoendelea ya uchambuzi wa sura ya kwanza na Sita katika Rasimu ya Katiba mpya.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati namba nne ya Bunge Maalum la Katiba, DKT Sira Ubwa Mamboya(kushoto) akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta(kulia) alipoitembelea Kamati hiyo jana mjini Dodoma kujionea kazi inayoendelea ya uchambuzi wa sura ya kwanza na Sita katika Rasimu ya Katiba mpya. Mwingine ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Christopher Ole Sendeka(katikati).
Mjumbe wa Kamati namba nne ya Bunge Maalum la Katiba, Dkt. Terezya Huvisa akiuliza swali wakati Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta(hayupo pichani) alipoitembelea Kamati hiyo jana mjini Dodoma kwa ajili kujionea kazi ya uchambuzi wa sura ya kwanza na Sita katika Rasimu ya Katiba mpya.
Mjumbe wa Kamati namba nne ya Bunge Maalum la Katiba, Mchungaji Christopher Mtikila akiuliza swali wakati Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta(hayupo pichani) alipoitembelea Kamati hiyo jana mjini Dodoma kwa ajili kujionea kazi ya uchambuzi wa sura ya kwanza na Sita katika Rasimu ya Katiba mpya. PICHA NA KAMATI YA BUNGE MAALUM LA KATIBA(BMK)

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa