Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WANAFUNZI nchini wametakiwa kutumia muda mwingi kujisomea katika maktaba ili kuongeza kiwango cha elimu na ufaulu.
Rai hiyo ilitolewa mjini hapa juzi na Mkuu wa Mkoa (RC) wa Dodoma,
Dk. Rehema Nchimbi kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya huduma za maktaba
Tanzania.
Mkuu huyo wa mkoa, alisema ili kiwango cha elimu kiongezeke nchini,
ni wajibu wa wanafunzi wote kwenda kujisomea katika maktaba.
Aliwataka wananchi kwenda mara kwa mara maktaba, kwani zipo kwa ajili ya watu wote sio kwa wanafunzi pekee.
Alieleza wasomi wengi wamekuwa wakifeli katika masomo yao kutokana na kuidharau na kutoitumia vizuri maktaba.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Injinia Lusako Kilembe,
alisema wanafunzi nchini wamekuwa hawana tabia ya kujisomea na kutafuta
maarifa, na badala yake hutumia muda mwingi kwenye mitandao na kufanya
mambo yasiyokuwa na maadili.
Chanzo;anzania Daima
0 comments:
Post a Comment