Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
IMEELEZWA kuwa mabalozi wa nyumba 10 wanaochaguliwa na Chama Cha
Mapinduzi (CCM) hawajui kusoma wala kuandika hali inayorudisha nyuma
maendeleo ya eneo husika.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, mjini Dodoma juzi Mwenyekiti
wa Mtaa wa Ilazo Kata ya Ipagala, Samwel Chimalusotola, alisema CCM
inachagua wajumbe wa nyumba 10 kisiasa.
“Tatizo la CCM wanaangalia kadi ya chama na mavazi ya chama hicho
hawaangalii upande wa elimu… nikiwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa
natekeleza sera za CCM,” alisema Chimalusotola.
Alishauri mabalozi wachaguliwe na wananchi badala ya chama ili wawe
chini ya wenyeviti wa serikali ya mtaa kwa lengo la kuleta maendeleo
yenye tija.
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment