Home » » MNYIKA AIBANA OFISI YA MAKAMU WA RAIS

MNYIKA AIBANA OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mbunge�wa Ubungo (Chadema) John Mnyika
 
Mbunge wa Ubungo (Chadema) John Mnyika, ameilipua ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) kuwa imetenga bajeti ya Sh. milioni 158 kwa ajili ya kufanya semina  katika mikoa kutetea mfumo wa Serikali mbili unaopigiwa debe na Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) (CCM).
Mnyika alisema juzi kuwa wakati wa uzinduzi wa mbio za Mwenge uliofanyika mkoani Kagera na kuzinduliwa na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal,   aliahidi ofisi yake  kujikita  katika kutoa elimu  kwa wananchi kuhusu Katiba mpya.

Alisema tayari Makamu wa Rais ameonyesha wazi msimamo wake wa Serikali mbili na katika bajeti yake ameongeza fedha za kutoa elimu hiyo kutoka Sh. milioni 126 hadi 158 fedha alizoziita zimeongezeka kwa ajili ya kujaza mafuta ya kueneza propaganda za Serikali mbili.

Mnyika alitoa tuhuma hizo wakati  akichangia katika kamati ya kupitia  makadirio ya matumizi ya bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano.

Alifafanua kuwa fedha hizo zimetengwa kwa ajili ya kufanya mabaraza ya ushauri ya wilaya (DCC) na Mkoa (RCC) vyombo ambavyo vinaongozwa na wakuu wa wilaya na mikoa ambao ni makada wa CCM wanaosimamia kuhakikisha mfumo wa Serikali mbili.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, badala ya Ofisi ya Makamu wa Rais kushughurikia kero za Muungano, lakini wameongeza pesa katika kipindi hiki kwa ajili ya kuzunguka, kwanini nisiamini kuwa wanaenda kuzunguka kwa ajili ya kueneza propaganda hizo za Serikali mbili kwa kutumia kodi za wananchi ninaondoa shilingi katika eneo hili” alisema Mnyika.

Mnyika alisema kama suala la kutoa elimu lifanywe na wafanyakazi wa ofisi hiyo badala ya viongozi wa kisiasa.

Akijibu hoja za Mnyika Waziri wa Muungano, Samia Hassan Suluhu, alisema kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi na wanasiasa kuhusu Muungano na si kampeni za CCM za kueneza Serikali mbili.
mwish
SOURCE: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa