Home » » MASHINDANO YA DARTS UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI YAFANYIKA DODOMA LEO‏

MASHINDANO YA DARTS UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI YAFANYIKA DODOMA LEO‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Mchezaji wa mchezo wa Vishale 'Darts' wa Timu ya Mbeya City, Mary Banabas (kushoto), akirusha mshale katika mashindano ya mchezo huo Ukanda wa Afrika Mashariki dhidi ya mchezaji Salome Gacheri wa Kenya, yaliyofanyika Viwanja vya Rose Garden mjini Dodoma leo. Mbeya City ilishinda kwa mabao 3-2.


 Mchezaji Levocatus Siriwa kutoka Magereza Jijini Arusha akirusha mshale katika mashindano hayo.
 Mchezaji kutoka Dodoma, Shukurani Dai akirusha mshale katika michuano hiyo.

 Mchezaji wa mchezo huo kutoka timu ya Lugalo Tanzania Mr Shawa akirusha mchale katika fainali hizo.
 Mzee Carlos Kidilu kutoka Dodoma akishiriki mchezo huo.
 Mchezaji Mr Herry kutoka Lugalo Dar es Salaam akirusha mshale.


 Mchezaji wa mchezo huo kutoka Dar es Salaam, Julius Mwiru akirusha mshale wakati wa mashindano hayo.
Wachezaji wa mchezo huo wakisubiri kushiriki michuano hiyo.

Dotto Mwaibale, Dodoma

SERIKALI imesema inampango wa kuanzisha mfuko maalumu kwa ajili ya kuendeleza michezo nchini.

Hayo yalibainishwa na Naibu Waziri wa Habari, Vijana  Michezo na Utamaduni, Juma Nkamia wakati akifungua mashindano ya mchezo wa Vishale ya Ukanda wa Afrika Mashariki'Darts' mjini Dodoma leo.

"Serikali inatarajia kuanzisha mfuko utakakuwa ikisaidia michezo yote hapa nchini ukiwemo huu wa Vishale" alisema Nkamia.

Alisema  mchezo wa mpira wa miguu ndio umekwa ukipewa kipaumbele zaidi lakini kupitia mfuko huo utasaidia michezo mingine ikiwemo wa Vishale ambao umekuwa maarufu hapoa nchini.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa Vishale Tanzania,David Msabi alisema wamekuwa na changamoto kubwa ya kukosa ufadhili kutoka serikalini na kuwa mchezo huo unaonekana unachezwa na walevi wakati si kweli.

Alitaja changamoto nyingine ni kukosekana kwa viwanja na walimu wa kufundisha mchezo huo ambao tayari utajitangaza kimataifa.

Katika mashindano hayo timu kutoka nchi za Uganda, Kenya zimeshiriki Tanzania ikiwa ni mwenyeji.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa