Home » » 1,550 WANG'ATWA NA MBWA WAZURURAJI

1,550 WANG'ATWA NA MBWA WAZURURAJI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

WAGONJWA 1,550 waliong’atwa na mbwa wanaozurura mitaani wamepokelewa katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma mwaka jana ambapo kati yao wanne walipoteza maisha.
Tangu kuanza kwa mwaka huu tayari watu sita wamepoteza maisha baada ya kung’atwa na mbwa wazururaji bila kupata chanjo baada ya kujeruhiwa.
Akizungumza na Tanzania Daima katika mahojiano maalum ofisini kwake, Mratibu wa huduma za chanjo na magonjwa yanayozuilika, Paul Mageni, alisema kuna ongezeko la watu kung’atwa na mbwa wazururaji Mkoa wa Dodoma.
Alisema katika hospitali hiyo wanapokea wagonjwa zaidi ya 10 kila siku huku akibainisha kwamba waliofariki walichelewa kupata chanjo ama hawakupata kabisa.
Kwa mujibu wa Mageni serikali ilikuwa ikitoa chanjo bure mara kwa mara lakini hivi sasa utaratibu huo hakuna kwa kuwa serikali imesitisha utoaji wa dawa za bure.
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa