Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe.
---
KIKAO cha
Bunge leo kimeanza kwa maswali kwa Waziri Mkuu ambapo aliyekuwa wa
kwanza kuuliza alikuwa ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,
Mhe. Freeman Mbowe
“…Chini
ya uongozi wako kama Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
ukiwa kiongozi wa shughuli za Kiserikali Bungeni, tumeiona Serikali
ikikumbana na matatizo na vikwazo vingi ikiwemo ‘Operesheni Tokomeza’
ambayo ilipelekea wananchi wengi kupoteza maisha na wengine kupata
vilema…“
Tumeona
mauaji ya raia yakiendelea Kiteto, kashfa kubwa ambayo iko current sasa
hivi ikiwa ni pamoja na kauli zako ulizowahi kuzisema kwamba fedha
zilizopotea za akaunti ya Escrow hazikuwa fedha za umma bali zilikuwa
fedha za watu binafsi…“– Mbowe.
Baada
ya Ripoti ya CAG kutolewa hadharani kuhusiana na fedha za Akaunti ya
Escrow na baada ya Ripoti ya PCCB kutolewa na hatimaye jana hapa Bungeni
kusomwa taarifa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), nini
msimamo wako kuhusu kauli yako ya awali kwamba fedha zile zilikuwa ni za
watu binafsi na sio fedha za umma?“– Mbowe.
Kwa
uzito huo ukichanganya na matukio mengine mbalimbali ambayo yamepelekea
fedheha kubwa kwa taifa letu, huoni kama ingekuwa muafaka kwako binafsi
na taifa kupumzika kidogo ili kupisha nafasi kwa watu wengine kuweza
kumalizia ngwe hii ya utawala wenu?”– Mbowe.
Akijibu
maswali hayo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema; “…Inawezekana
Mheshimiwa Mbowe una shauku ya kutaka litokee hilo lakini mambo haya
yanategemea kama ndivyo Mungu kapanga au hapana…“
Ningeweza
nikajaribu kukujibu lakini sina sababu ya kufanya hivyo, sina sababu ya
kufanya hivyo kwa sababu suala lenyewe ndiyo subject ya mjadala hapa
Bungeni ambao unaanza leo.. Tusubiri mjadala utakavyokwenda naamini na
mimi nitapata nafasi ya kusema mawili matatu, kwa hiyo nadhani mwisho wa
yote Bunge litakuwa limefikia mahali ambapo tunaweza tukasema kwa
uhakika ni hatua stahiki namna gani inaweza kuchukuliwa…” Waziri Mkuu
Mizengo Pinda.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment