MBUNGE wa Mbeya Vijijini, Mchungaji Lackson Mwanjali ameanguka ghafla katika eneo la Bunge, mjini hapa jana.
Mbunge huyu, alipatwa na mkasa huo jana majira ya saa sita mchana.
Walioshuhudia tukio hilo, waliiambia Tanzania Daima kuwa, Mbunge huyo wa CCM alianguka wakati akienda maliwatoni.
“Alikuwa anatoka ukumbini kwenda kwenye ‘kantini’ ya Bunge, lakini kabla ya kuingia alitaka kwenda maliwatoni na kabla ya kuingia, alianguka,” alisema mmoja wa walinzi waliombeba Mbunge huyo.
Mbunge huyo alikimbizwa katika hospitali ya Bunge na baadaye kukimbizwa hospitali ya mkoa ambako amelazwa.
Haikuweza kujulikana mara moja sababu ya kuanguka kwa mbunge huyo, ingawa muuguzi mmoja wa hospitali ya Bunge alisema alikuwa anasumbuliwa na homa kali.
Chanzo;Tanzania Daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment