Sheikh
Shariff Matongo akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake
jijini Dar es Salaam (hawapo pichani)kuhusu ndoto yake ambayo
ameoteshwa kuelekea mwaka 2015.
NA CHALILA KIBUDA,GLOBU YA JAMII,DAR.
Sheikh
Sharif Matongo amesema ameoteshwa ndoto ya mwaka 2015 na kupata ushauri
kwa mashekh mbalimbali Duniani ambavyo vitatokea nchini na viongozi
wasipuuze ndoto hiyo. Sharif aliyasema hayo leo ofisini kwake
alipokutana na waandishi wa habari ,alisema ameoteshwa mambo saba
likiwemo la kupata Rais ajaye ambaye kiongozi ambaye muda mwingi ameishi
nje ya nchi kwa kufanya kazi.
Alisema
katika ndoto nyingine kifo cha kiongozi mkubwa ambaye ameshika
nyadhifa mbalimbali na mwenye kambi katika Chama cha Mapinduzi (CCM). Sheikh
alisema ndoto nyingine kutokea kwa mvua nyingi ambapo watu wanaoishi
mabondeni ,kutokea kwa vifo vya watoto vingi ,wafanyabiashara kupata
mafanikio makubwa kwa mwaka utaoanza kesho.
Vijana
wengi watashinda katika uchaguzi ujao na wazee wataangushwa sana hivyo
wanatakiwa kujitokeza,katiba inayopendekezwa itapita lakini kutakuwa na
vurugu ambazo zitaibuliwa na vijana.
‘’Ndoto
yangu niliooteshwa sikukaa nayo peke yangu, niliweza kupata ushauri
kutoka kwa watu mbalimbali akiwemo Mufti wa Abhu Dhabi,Mufti wa
Nigeria na wengine wote wakaniambia suala hilo nisikae
nalo,niwashirikishe na Watanzania wenzangu’’alisema Sheikh Shariff
Matongo.
Sheikh
Shariff alisema katika usafiri wa bahari utakuwa mbaya kutokana na
bahari kuchafuka na chombo kimoja kitazama kutokana na kuchafuka huko.
Alisema
ndoto hizo ni lazima kuzingatia kutokana na kupata ushauri wa watu
wengi wenye kuaminika katika jamii katika mataifa mbalimbali
ulimwenguni.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment