Home » » UKWELI KUHUSU AFYA YA NAIBU SPIKA NDUGAI HUU HAPA

UKWELI KUHUSU AFYA YA NAIBU SPIKA NDUGAI HUU HAPA




                _____________         

Kumekuwa na taarifa zinazosambazwa kwenye Mitandao ya kijamii kuhusu hali  ya Afya ya Naibu Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai. Ofisi ya Bunge inapenda  kuutangazia umma na Wananchi wote kuwa, taarifa hizo zinazosambazwa katika baadhi  ya Mitandao si za kweli, bali ni uzushi mtupu.

   

Ukweli ni kwamba Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai ni Mzima wa afya na  hivi sasa yuko jimboni kwake Kongwa, Mkoani Dodoma akifanya maandalizi


 ya Mwisho  ya Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana itakayofanyika mwishoni  mwa wiki hii na hasa Jimboni Kongwa, Dodoma.

    

 Ofisi ya Bunge inapenda kuwatoa hofu Wananchi wote na kuwataka kuzipuuza taarifa hizo kwa kuwa si za kweli bali ni uvumi unaonezwa na watu wachache wenye nia ovu ya  kujenga hofu miongozni mwa Wananchi kupitia mitandao ya kijamii.



Aidha tunapenda kutoa rai kwa watu wote kuacha kusambaza taarifa hizo potofu na  badala yake kama kuna taarifa zozote kuhusu Ofisi ya Bunge au Viongozi wake wafanye jitihada za kuthibitisha taarifa hizo kwenye Mamlaka husika kabla za kuzisambaza. Ofisi ya Bunge inao utaratibu rasmi wa kutoa taarifa muhimu kwa wananchi na umma kwa ujumla, hivyo si vyema kwa watu kusambaza taarifa potofu kuhusu Bunge na  viongozi wake ambazo zinaweza kuleta usumbufu miongoni mwa Viongozi na baadhi ya  wananchi.



 Imetolewa na:    Idara ya      Habari,       Elimu         kwa   Umma        na      Uhusiano   wa          Kimataifa   Ofisi ya      Bunge        DAR         ES     SALAAM 





4       MACHI     2015

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa