Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Urban
Epimark,Mpwawa.
HALMASHAURI ya Wilaya ya Mpwawa
imekanusha vikali taarifa kwamba BARAZA LA Madiwani wa Halmashauri hiyo limetunga
sheria mpya ya tuzo mbalimbali kinyemela ili kuwazibiti wafanyabiashara
wanaoegemea upande wa upinzania.
Hayo yalielezwa juzi na Kaimu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mpwawa, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya
Chunyu, Mhe Neemia Kongawadodo kwenye mikutanao ya hadhara iliyofanyika katika
kata za Mlunduzi, Luhundwa na Wota Jimbo la Kibakwe wilaya ya Mpwawa.
Diwani huyo aliyemwakilisha
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe Alex Buramulete Nyaulingo aliwaambia
wananchi kwamba, hakuna sheria yeyote iliyotungwa na kupitishwa na Baraza la
Madiwani hivi karibuni inayokusudia kutoza malipo kwa wananchi mbalimbali wanaojihusisha
na biashara za bodaboda, mafundi pikipiki na baiskeli, mama na babalishe au
tozo za uvunaji miti au mbao.Alisema hizo ni mbinu za baadhi ya watu
wasioitakia mema halmashauri hiyo katika utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha
Mapinduzi ambapo baraza hilo la Madiwani lote lipo chini ya mwavuli wa Chama cha
Mapinduzi.
Aliendelea kusema, baraza hilo
limekuwa siku zote likitunga na kupitisha sheria ndogondogo katika halmashauri
hiyo na kuziweka wazi hadharani kwa kufuata taratibu za kisheria zilizowekwa, sasa
iweje muda unafikia mwisho wa utekelezaji wa Ilani yake, yaanze kuibuka
malalamiko kama hayo. Alieleza Diwani Kongawadodo.
Nae Katibu Mwenezi wa Chama Cha
Mapinduzi Wilaya ya Mpwawa Bw Origenesi John alikitetea chama kwa kueleza
kwamba, “wale wote wenye tamaa ya kuwania baadhi ya nafasi za uongozi kwa ngazi
ya Udiwani na Ubunge katika uchaguzi mkuu ujao kupitia Chama Cha Mapinduzi
kuacha kufanya hivyo sasa kwani muda wa kamapeni bado haujaanza.
Alisema, “waacheni madiwani wetu
pamoja na wabunge watekeleze kwa ukamilifu jukumu walilokabidhiwa na chama,
bila kuwaingilia”. Aliendelea kusema huku akinukuu vifungu vya kanuni za
uchaguzi kwenye katiba ya CCM kwamba, wanaofanya hivyo wanajipunguzia sifa za
kuwa wagombea, na wakati ukifika watapoteza sifa za kuteuliwa.
Aliendelea kuainisha kwamba, CCM
imegundua inao wanachama wengi wanaokusudia kuwania nafasi mbalimbali kwenye
uchaguzi ujao, lakini amewashauri wavute subira hadi muda utakapofika. “Kuendelea
kupotosha wananchi kwa kutoa kauli au shutuma kwa viongozi waliopo madarakani
hivi sasa hakutasaidia, kwani hali halisi inajidhiirisha kwamba chama kwa
kushirikiana na wabunge wao na madiwani wamefanya mambo mengi na makubwa, hivyo
wasijidanganye”, alieleza katibu mwenezi huyo.
Aliendelea kuainisha jinsi
walivyoshirikiana na halmashauri ya Mpwawa pamoja na Mbunge wao wa Kibakwe, Mhe George Simbachawene, ambaye pia
ni Waziri wa Nishati na Madini kuwaletea wananchi maendeleo katika maeneo
mbalimbali ya jimbo hilo ikiwemo ukarabati wa barabara, usambazaji wa umeme
kupitia REA, ujenzi wa shule na maabara, ujenzi wa zahanati na kuhakikisha
upatikanaji wa vifaa tiba husika na mengine mengi.
Aliendelea kueleza katika mikutano
hiyo, ambapo yeye alijigamba kuendelea “kuporomosha mawe ya ukweli kwa
wapinzania” kwamba ukarabati wa gari la shule ya sekondari ya Wota iliyopo Kata
ya Wota, Jimbo la Kibakwe, uliofanikishwa kwa kiwango cha juu kabisha na mbunge
wa Jimbo hilo, ambapo gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser lenye usajili Na.
STJ 5656 la Shule ya Sekongari ya Wota, lilikaa gereji kwa miaka 5 kutokana na ukosefu wa
fedha za kulikomboa lakini Mbunge huyo kwa kusaidiana na wananchi wa Kibakwe
wamefanikiwa kulipa na kukuomboa gari hilo baada ya kulipia gharama ya shilingi
milioni 17, na sasa amelikabidhi kwa Mkuu wa shule hiyo.
Aliendelea kuwapinga wapinzani
kwamba, usambazaji wa umeme katika kata hizo pamoja na ujenzi wa zahanati ya Wota, ujenzi
wa barabara za kutoka Kibakwe mjini hadi maeneo mbalimbali ya Kata za
Mlunduzi,Luhundwa na Wota pamoja na upatikanaji wa dawa kwenye zahanati husika,
ni salamu tosha kwamba CCM imetekeleza vyema ahadi zake za kuwaletea wananchi
maisha bora kwa kila mtanzania, hivyo wasiwabeze viongozi waliopo madarakani
hivi sasa, alieleza.
Chama cha Mapinduzi wilaya ya
Mpwawa, kilijumuika katika ziara ya
mbunge wa Jimbo la Kibakwe, kukagua maendelea ya miradi mbalimbali ya
maendeleo inayotekelezwa chini ya Ilani ya chama, ikiwamo mradi wa usambazaji
umeme vijijini kupitia REA. Mafanikio makubwa yamefikiwa na TANESCO hadi sasa katika
harakati za kusambaza umeme vijijini.
0 comments:
Post a Comment