Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Urban
Epimark,Dodoma
Wito umetolewa kwa Halmashauri
zote nchini kupanga utaratibu wa kumilikisha na kutoa leseni za uchimbaji
madini kwenye serikali za vijiji kwenye maeneo yatakayogundulika kuwa na madini
ili mapato hayo yaweze kusaidia serikali za vijiji kuendeleza huduma za kijamii.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa
Nishati na Madini Mh George Simbachawekene, ambae pia ni Mbunge wa Kibakwe
alipokuwa akitembelea maendelea ya usambazaji umeme vijijini (REA) hivi
karibuni katika wilaya ya Mpwawa.
Waziri akiambatana na maofisa ya
Wizara ya hiyo upande wa Madini na Nishati, alisema maeneo mengi kwa sasa yamegundulika
kuwepo na madini mbalimbali yakiwamo yenye thamani ya juu na ya chini ikiwamo
wilaya ya Mpwawa. Amezishauri serikali zote za vijiji nchini kushirikiana na
maofisa wa madini walio katika kanda zao ili wawasaidie kuyatambua madini hayo
na kuwapatia leseni za kuyachimba kama vijiji na si mtu binafsi.
Nae Kamishna wa Madini Kanda ya
Kati, Injiania Sothenes Massola aliwaambia wananchi wa maeneo hayo ya Mpwawa
kuwa, wilaya yao imegundulika kuwa na baadhi ya madini mengi yakiwamo shaba, rubi
na chokaa pamoja na mawe, mchanga na udongo mzuri kwa ajili ya ujenzi wa
barabara na majumba ambazo zote ni madini kulingana na utaratibu. Amesema,
Ofisi ya Madini Kanda ya Kati itaanda ziara ya kutembelea wanakijiji wote
maeneo hayo hususani yenye madini na kutoa elimu ya jinsi ya kuyatambua madini
hayo na taratibu za kupatiwa leseni ili wasidhulumiwe na wajanja wachache.
Wananchi wa wilaya hiyo ya Mpwawa
walivutiwa na ziara ya hiyo ya Waziri na kumwomba awasaidie haraka ili vijiji
vyao viweze kupatiwa leseni na elimu ya kutambua madini hayo. Walieleza kwamba
endapo watapatiwa uelewa wa shughuli za madini, vijana wengi watajihusisha na
kazi hiyo na kuondoa tatizo la umaskini unaolikabili taifa.
Waziri pia amelipongeza shirika
la umeme nchini, TANESCO kwa kusimamia vizuri kasi ya usambazaji umeme vijijini
kwa kushirikiana na wakala wa umeme vijiji yaani REA.
Meneja wa Tanesco Kanda ya Kati
Injiani Joeli Kuandika, alimweleza Waziri kwamba, watahakikisha kasi ya
usambazaji umeme maeneo yaliyokusudiwa wilaya ya Mpwawa yatawaka umeme kama
ilivyopangwa kwa kushirikiana na REA kwani hadi sasa kasi ya usambazaji inaenda
vizuri.
0 comments:
Post a Comment