Home » » BUNGE LA BAJETI KUANZA KUJADILI MISWADA SABA

BUNGE LA BAJETI KUANZA KUJADILI MISWADA SABA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Bunge la Bajeti litaanza kujadili miswada saba kwa siku 10 kuanzia Juni 29 hadi Julai 8, mwaka huu.
Mkutano huo wa 20 wa Bunge la 10 ni wa mwisho katika chombo hicho cha kutunga sheria kabla ya kuvunjwa, kupisha Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Mwenyekiti wa Bunge, Kidawa Hamid Saleh alisema jana kuwa baadhi ya miswada hiyo inakuja kwa mara ya kwanza.
Kwa mujibu wa tovuti ya Bunge, Miswada hiyo ni wa Sheria ya Kupata Habari wa Mwaka 2015 ambao utasimamiwa na Kamati ya Maendeleo ya Jamii na utakuja bungeni kwa mara ya pili.
Mara ya kwanza ulitajwa kwenye Bunge la 10 katika mkutano wa 19.
Miswada inayokuja kwa mara ya kwanza ni; Sheria ya Tume ya Walimu ya mwaka 2015 ambao utasimamiwa na Kamati ya Huduma za Jamii.
Muswada mwingine ni wa Sheria ya Kufuta Benki ya Posta wa mwaka 2015 utakaosimamiwa na Kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara.
Mwingine ni wa Sheria ya Kituo cha Pamoja Mipakani wa mwaka 2015 utakaosimamiwa na Kamati ya Miundombinu wakati wa Sheria ya Taasisi ya Petroli na Gesi wa mwaka 2015, utakuwa chini ya Kamati ya Nishati na Madini.
Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi wa Mwaka 2015 utasimamiwa na Kamati ya Nishati na Madini, huku wa Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji Tanzania katika Tasnia ya Uziduaji wa mwaka 2015 ukiwa chini ya Kamati ya Nishati na Madini.
Akifungua Mkutano Mkuu wa Tano wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Arusha hivi karibuni, Rais Jakaya Kikwete alisema miswada itakayojadiliwa mmojawapo ni wa kuanzishwa Tume ya Utumishi ya Walimu.
Rais Kikwete alisema tume hiyo itawezesha walimu kuwa na chombo kimoja cha kuwasimamia.
Hata hivyo, Mwananchi ilidokezwa kuwa moja kati ya miswada itakayowasilishwa na Serikali ni pamoja na wa marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi
Chanzo:Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa