Home » » SERIKALI YAWASILISHA MISWADA 7 BUNGENI

SERIKALI YAWASILISHA MISWADA 7 BUNGENI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


SERIKALI imewasilisha bungeni Mjini Dodoma, Miswada saba ya Sheria ili iweze kujadiliwa, kupitishwa na Bunge ukiwemo 
wa kuifuta Benki ya Posta.

Miswada hiyo iliwasilishwa na Makatibu wa Bunge, Ramadhani Issa na Asia Minja ambayo itaanza kujadiliwa na kupitishwa 
katika hatua zake zote ifikapo Julai 8, mwaka huu.

Mbali ya Muswada huo, mingine ni Muswada wa Sheria ya Tume ya Walimu wa Mwaka 2015, Muswada wa Sheria ya Kituo cha Pamoja Mipakani wa Mwaka 2015 na  Muswada wa Sheria ya Taasisi ya Petroli na Gesi wa Mwaka 2015.

Mingine ni Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi wa Mwaka 2015, Muswada wa Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji Tanzania katika Tasnia ya Uzinduaji wa Mwaka 2015 na Muswada wa Sheria ya Kupata Habari wa 2015. 

Muswada wa Sheria ya Kupata Habari nao utajadiliwa na Bunge kwa mujibu wa iliyotolewa kwa umma kupitia tovuti ya Bunge ambayo iliwataka wadau mbalimbali kutoa maoni yao katika kamati zilizowekwa kwa ajili ya kupokea maoni yao.

Awali kwa mujibu wa ratiba, Bunge lilitakiwa kumalizika Juni 27, mwaka huu, lakini kutokana na miswada hiyo saba, muda 
umeongezwa sasa litamalizika Julai 8, mwaka huu.

 Chanzo:Majira


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa