Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Viongozi wa juu wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba
 ya Wananchi (Ukawa), akiwamo aliyekuwa mgombea urais wa Tanzania 
kupitia Chadema, Edward Lowassa na wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif 
Hamad, walijifungia mjini hapa jana kujadili mambo mawili mazito.
Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia Nipashe kutoka vyanzo vyetu vya
 ndani, viongozi hao walijadili mustakabali mzima kuhusu kutangazwa 
kurudiwa kwa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar Machi 20, mwaka huu pamoja na 
uamuzi wa wabunge wao kugomea Kamati za Bunge.
Aidha, viongozi hao baada ya kufia uamuzi, jana usiku walikuwa na 
mkutano na wabunge wa Ukawa kuwaeleza uamuzi waliofikia na nini 
wanachotakiwa kukifanya wakiwa bungeni.
"Ni kweli viongozi wa juu wamejadili mambo makubwa mawili, hatma ya
 uchaguzi wa Zanzibar na kuhusu Kamati za Bunge zilivyoundwa, subiri 
kidogo tukitoka katika kikao nitakueleza kila kitu," kilieleza chanzo 
chetu. 
     CHANZO:
     NIPASHE
    
0 comments:
Post a Comment