Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.
Mhe Eng Godwin Ngonyani akijibu maswali ya wabunge katika kikao cha
Bunge la 11linaloendelea Mjini Dodoma. picha na Raymond Mushumbusi
MAELEZO
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Serikali imeahidi kuendelea na ujenzi wa barabara katika maeneo tofauti
nchini kwa kiwango cha lami ili kutatua adha kubwa ya ubovu wa barabara
ulipo katika maeneo mengi nchini.
Hayo yamesemwa leo Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.
Eng Godwin Ngonyani akijibu maswali ya wabunge waliouliza kuhusu mpango
wa serikali kuboresha barabara zilizopo na kujenga mpya ili kukabiliana
na adha ya ubovu wa barabara nchini.
Akijibu swali la Mhe Richard Mganga Ndassa Mbunge wa Sumve (CCM) lililohitaji ufafanuzi
wa serikali ni lini ujenzi wa barabara ya Magu-Bukwimba
–Ngudu-Hungumalwa itajengwa kwa kiwango cha lami, Mhe Eng Godwin
Ngonyani amesema katika mwaka
wa fedha 2014/15 na 2015/16 serikali ilitenga jumla ya shilling
millioni 200 kwa ajili ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa
barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 70 na taratibu za kumtafuta
Mhandisi Mshauri zinaendelea na baada ya kukamilika kwa usanifu na
kupata gharama za mradi huo, Serikali itatafuta fedha za kuanza ujenzi
wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.
Aidha akijibu pia swali la Mhe Fredy Atupele Mwakibete Mbunge
wa Busokelo (CCM) aliyehitaji kujua ni lini barabara ya
Katumba-Mbambo-Tukuyu yenye urefu wa Kilometa 82 inayoanzia Katumba(RDC)
kupitia Mpombo,Kandete,Isange,Lwanga, Mbambo (BDC) hadi Tukuyu (RDC)
itajengwa kwa kiwango cha lami.
Akijibu swali hilo, Mhe. Eng Godwin Ngonyani amesema kuwa Serikali kupitia Wakala
wa Barabara (TANROADS) kwa kutambua umuhimu wa barabara hii, katika
mwaka wa fedha 2009//10 Serikali ilianza maandalizi ya ujenzi wa
barabara hii kwa kiwango cha lami na ambapo upembuzi yakinifu na sanifu
wa kina ulikamilika na baadae Serikali iliamua kujenga kilometa 10
ambapo mwezi April,2014 Wakala wa Barabara na kampuni ya CICO ilijenga
barabara hiyo kuanzia Lupaso hadi Buseji,Wilayani Busokelo.
Serikali kupiti Wakala wa Barabara (TANROADS) inaendelea na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha
lami katika Kata, Wilaya na Mikoa mbalimbali nchini ili kukabiliana na
adha ya ubovu wa barabara ambao umesababisha watu kukosa mawasiliano
baina ya maeneo.
0 comments:
Post a Comment