Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Serikali
imetolea ufafanuzi kuhusu taarifa za upotoshaji kwa umma kuwa imefuta
vipindi vya shughuli za Bunge kuoneshwa katika televisheni ya Shirika la
Utangazaji la Tanzania (TBC) kama zisemazo taarifa zilizozagaa mitaani.
Hayo
yamesemwa leo Mjini Dodoma na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na
Michezo Mhe.Nape Mose Nnauye wakati akiongea na wananchi moja kwa moja
kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini kutolea ufafanuzi taarifa za
upotoshaji juu ya TBC kufuta vipindi vya matangazo ya vikao vya Bunge.
Mhe.Nape
Moses Nnauye amesema Serikali haijafuta vipindi vya Bunge bali
ilichofanya ni kubadilisha muda wa kurusha vipindi hivyo kutoka muda wa
mchana na kuviweka usiku kwa lengo la kupunguza gharama za kurusha moja
kwa moja matangazo hayo ya Bunge na pia kuwapa fursa wananchi zaidi
kuangalia na kufatilia yanayoendelea Bungeni kwa kuwa muda wa usiku watu
wengi wanakuwa wamesharejea kutoka katika shughuli zao za ujenzi wa
taifa.
Ameongeza
kuwa Serikali imechukua uamuzi wa busara katika hili kwani TBC imekuwa
ikitumia Sh Billion 4.2 kwa mwaka kama gharama za urushaji wa moja kwa
moja wa matangazo hayo , hivyo itasaidia katika kubana matumizi ya
shirika hilo kwani fedha hizo hazipo katika bajeti ipewayo shirika bali
ni fedha za ndani zinazokusanywa na shirika hilo.
Aidha amesema kuwa sio kitu kigeni kwa Bunge kutotangazwa moja kwa
moja kwani kuna baadhi ya mabunge katika nchi nyingine urekodiwa na
kurushwa baadae kama kipindi maalum cha Bunge,amezitaja baadhi ya nchi
hizo kuwa ni New Zealand, India, Malawi, Lesotho, Uingereza na
Singapore.
Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) lilianza kurusha matangazo
ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
mwaka 2005 ila baada ya Serikali kukaa na kujadili kwa kina kuhusu
gharama za urushaji wa matangazo hayo moja kwa moja ikaamua kubadili
mtindo wa urushaji wa matangazo hayo kutoka matangazo ya moja kwa moja
kwa siku nzima kwenda kwenye mfumo wa kuyarekodi na kuyarusha katika
kipindi cha LEO KATIKA BUNGE.
0 comments:
Post a Comment