Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
amesema kwamba matangazo ya bunge hayatarushwa yote live kama serikali
ilivyosema na tayari hatua hiyo imekwisha kuanza.
Majaliwa ameyasema hayo
alipokuwa akijibu swali la papo kwa papo la Mbunge wa Hai ambaye pia ni
msemaji wa kambi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe aliyetaka kujua
kwanini serikali imefanya maamuzi ya kuzuia wananchi wasione matangazo
ya Bunge moja kwa moja.
Akijibu swali hilo Waziri
Mkuu amesema kwamba uamuzi wa kutoonyeshwa kwa matangazo ya moja kwa
moja uliombwa na chombo cha umma chenyewe kwamba hakina uwezo
kujiendesha na uamuzi wao huo umeungwa mkono na serikali.
''Maamuzi ya chombo hiki
yameungwa mkono na serikali na waziri amefanya kipindi maalum kuhusiana
na jambo hilo na wananchi wameelewa vizuri na wameiunga mkono serikali
kwamba matangazo yatarekodiwa na yatarushwa kama kipindi maalum
usiku''Amesema Waziri Majaliwa.
Aidha chombo cha umma
kitakuwa kinarusha matangazo ya moja kwa moja kwa muda wa maswali na
majibu kwa serikali na baada ya hapo matangazo yatarekodiwa na kuruswa
katika kipindi kiitwacho leo katika Bunge.
0 comments:
Post a Comment