Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba,
amewaagiza viongozi kuhakikisha wale wote waliohusika na wizi wa fedha
za wakulima kufikishwa mahakamani mara moja.
Alitoa agizo hilo bungeni jana wakati akijibu swali la nyongeza la
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, aliyehoji kuhusiana na ripoti ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2013
iliyoelezea upotevu wa Sh. bilioni 28 za wakulima wa zao la tumbaku
mkoani Tabora.
Nchemba alisema hiyo ripoti anaifahamu na kuagiza wale wote waliohusika katika kuwaibia wakulima hao kuchukuliwa hatua.
Alisema suala hilo halipo kwenye tumbaku tu, kwani kuna maeneo
mengine ambayo yana changamoto hiyo ya wakulima kuibiwa fedha zao na
kuahidi kuwashughulikia wote waliohusika baada ya Bunge kumalizika.
Alisema serikali imepanga kupitia makato yote yanayokatwa kwa wakulima na ndani ya siku mbili atatoa tamko juu ya suala hilo.
Nchemba alisema Rais John Magufuli ameshaonyesha kukerwa na tozo
nyingi za makato kwa wakulima, hali ambayo inawafanya wakose maendeleo,
hivyo atalishughulikia suala hilo kwa wakati.
SOURCE:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment